Skip to main content

Mwalimu chupuchupu kuuawa na wananchi, wenzake wamnusuru kwa kumfungia na kufuli ofisini

Mwalimu wa Shule ya Msingi Mitonji katika Kijiji cha Mitonji Kata ya Mbuyuni katika Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, John Mandanda amenusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kali, baada ya kuwacharaza viboko wanafunzi hadi mmoja kupoteza fahamu.
Image result for waziri wa elimu
Mwanafunzi huyo wa darasa la sita (jina linahifadhiwa) anadaiwa kupoteza fahamu kwa zaidi ya saa moja.
Kutokana na tishio la kuchapwa na wananchi hao walimu walimwokoa mwenzao kwa kumfungia ndani ya ofisi, huku wananchi hao waliotaka kumpa kichapo wakiwa wamebeba marungu, mashoka na silaa zingine za jadi.
Akizungumza na Nipashe jana kwa njia ya simu, Ofisa Elimu Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Elizabeth Mlaponi, alisema mwalimu huyo alifanya tukio hilo juzi majira ya saa 5:00 asubuhi wakati wanafunzi walipokuwa wakiingia darasani baada ya mapumziko mafupi.
Alisema mwalimu huyo akiwa shuleni hapo siku ya tukio, alitoa adhabu kwa baadhi ya wanafunzi ambao inaelezwa kuwa wanafunzi hao walikuwa wamechelewa kuingia darasani baada ya kengere ya kuingia darasani kupigwa, huku wakiwa nje ya darasa.
Mlaponi alisema mwalimu huyo baada ya kuona wanafunzi hao wamechelewa kuingia darasani, aliamua kuwacharaza viboko wanafunzi hao kila mmoja viboko viwili.
Alisema baada ya kutoa adhabu ndipo mmoja wa wanafunzi hao baada ya kuchapwa kiboko kimoja alianguka chini ya sakafu na na kumsababishia majeraha kwenye baji la uso wake.
“Tulipopata taarifa juu ya tukio hili la mwalimu kumchapa mwanafunzi na kumsababishia majeraha, tulifika hadi shuleni hapo na tulikuta wananchi wamezingira eneo la ofisi ya mwalimu mkuu ambapo alikuwa amefungiwa ndani na walimu wenzake wakimataka mwalimu huyu atolewe nje ili wampige,”alisema Mlaponi.
Afisa elimu huyo alieleza kuwa suala la mwalimu huyo wanaendelea kulishughulikia ikiwa ni pamoja na kulepeka katika ngazi za juu ikiwamo ofisi ya mkuu wa wilaya kwa ajili ya utekelezaji zaidi.
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Mitonji, Shabani Nguseka, alisema ofisi ya serikali ya kijiji na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mitonji walipata taarifa hizo kutoka kwa baadhi ya wanafunzi wenzake wa shule hiyo wakieleza kuwa mwenzao amepigwa hadi kuzimia.
Mguseka alisema baada ya wananchi kupata taarifa hizo waliandamana hadi shuleni hapo na wakishinikiza kutaka mwalimu huyo wampe kichapo kama alivyomchapa mwanafunzi hadi kumsababishia kupoteza fahamu.
Alisema uongozi wa serikali ya kijiji ulishirikiana na familia ya mwanafunzi huyo kwa kumchukua mwanafunzi kumpeleka kwenye Zahanati ya kijiji cha Nagaga kwa ajili ya kupata matibabu ya awali.
Baba mdogo wa mwanafunzi huyo, Emmanuel Asili, alisema baada ya kupata taarifa hizo kuwa mtoto wake amepoteza fahamu baada ya kuchapwa kiboko, alilenda shuleni na kumkuta mwanae amepoteza fahamu, lakini alipoona akitokwa damu puani na masikioni ndipo alipochukua hatua za kumpeleka katika Zahanati ya Nagaga na baadae hospitali ya mji Masasi Mkomaindo.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu mwalimu Mandanda ambaye ndiye aliyemchapa kiboko mwanafunzi huyo, alikiri alifanya kitendo hicho, lakini alisema alimcharaza kiboko kimoja.
“Ni kweli nilimchapa kiboko kimoja na baada ya kumchapa nilimsikia akitamka maneno ambayo yalikuwa kama ni matusi hivi ndipo nilipopandwa na hasira, hivyo nikaanza kumpiga kwa kutumia mateke hivyo akaanguka sakafuni na kupata majeraha hayo,”alisema Mandanda.
Mandanda alisema ameamua kubeba gharama zote za matibabu za mwanafunzi huyo hadi pale atakapopata nafuu, na kwamba kutokana na tishio la kudhuriwa, ameamua kujificha yeye na familia yake.

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji watatu PSG wakutwa na corona

  Mshambuliaji wa timu ya Paris Saint-Germain,  Neymar de Santos,   ameripotiwa kukutwa na virusi vya corona pamoja na wachezaji wengine watatu. Hata hivyo  Paris Saint-Germain  ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Ufaransa na kumaliza nafasi ya pili kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, wameshindwa kuwaweka wazi wachezaji hao wengine ambao wamekutwa na virusi hivyo. Lakini  Angel Di Maria  mwenye umri wa miaka 32 na Leandro Paredes mwenye miaka 26, wanatajwa kuwa kati ya wachezaji hao kwa mujibu wa L’Equipe. Mara baada ya Paris Saint-Germain kumaliza mchezo wa mwisho wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich, Agosti 23, wachezaji hao watatu walionekana kuwa pamoja kwenye visiwa vya Ibiza wakiponda raha ambapo ni Neymar, Di Maria na Paredes.

MWONGOZO WA USAFIRISHAJI WA BIDHAA MUHIMU NA HUDUMA KATIKA NCHI ZA SADC KWA KIPINDI HIKI CHA JANGA LA VIRUSI VYA CORONA

Tarehe 6 Aprili, 2020 ulifanyika Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).  Mkutano huo ulijadili janga la mlipuko wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu (COVID-19) unaosababishwa na virusi vya Corona. Mkutano huo ulihusisha Mawaziri wenye dhamana ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Fedha,Viwanda,Biashara, Utalii, Mambo ya Ndani na Uchukuzi, kutoka nchi 16 wanachama wa SADC ambazo ni Angola, Botswana, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Jamhuri ya Visiwa vya Ushelisheli, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Zambia. Katika mkutano huo, Baraza la Mawaziri lilitoa mwongozo kuhusu Usafirishaji wa Bidhaa Muhimu na Huduma Katika Nchi za SADC katika kipindi hiki cha janga la Virusi vya Corona.  Mwongozo huu utatumika katika kipindi hiki unalenga kupunguza safari zisizo za lazima na usafirishaji wa bidhaa ambazo ni za muhimu tu na unazitaka Nchi Wanachama kuzingatia na kutekeleza sera na miongozo mbalimbali

Mambo muhimu ya kuzingatia unapohitaji kufanikiwa

Wengi wetu mara nyingi huwa tunafikiri kukosa mafanikio ni matokeo ya kukosa bahati katika maisha. Fikra hizo mara nyingi, huwazuia  wengi katika kufanikiwa na kujikuta wakiishia kuwa  watu wa kulaumu na kushindwa kila siku. Kimsingi  kitu kikubwa kinachochangia kuzuia mafanikio yetu ni baadhi ya tabia tulizo nazo. Si kweli kwamba watu wengi hushindwa kuendelea kutokana na kukosa mitaji bali ni kwa sababu ya tabia zao. Tabia ni kikwazo kikubwa cha maendeleo ya mtu binafsi kuliko unavyodhani. Zingatia haya yafuatayo ikiwa unahitaji kufanikiwa katika maisha yako:- Epuka kufikiria sana juu ya makosa uliyoyafanya. Kama kuna sehemu ulikosea katika siku za nyuma, hiyo imeshapita chukua hatu za kusonga mbele. Acha kutumia muda wako mwingi na kufikiri pale ulipokosea kwani hiyo haitakusaidia zaidi ya kukurudisha nyuma. Kumbuka kuwa kukosea ni sehemu ya maisha ya binadamu, kitu cha msingi jifunze kutokana na hayo makosa. Usiwe mtu wa kuongelea ndoto zako kila siku. Wengi