Skip to main content

Wachezaji watatu PSG wakutwa na corona

 

Mshambuliaji wa timu ya Paris Saint-Germain, Neymar de Santos, ameripotiwa kukutwa na virusi vya corona pamoja na wachezaji wengine watatu.

Hata hivyo Paris Saint-Germain ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Ufaransa na kumaliza nafasi ya pili kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, wameshindwa kuwaweka wazi wachezaji hao wengine ambao wamekutwa na virusi hivyo.

Lakini Angel Di Maria mwenye umri wa miaka 32 na Leandro Paredes mwenye miaka 26, wanatajwa kuwa kati ya wachezaji hao kwa mujibu wa L’Equipe.

Mara baada ya Paris Saint-Germain kumaliza mchezo wa mwisho wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich, Agosti 23, wachezaji hao watatu walionekana kuwa pamoja kwenye visiwa vya Ibiza wakiponda raha ambapo ni Neymar, Di Maria na Paredes.

Comments

Popular posts from this blog

MWONGOZO WA USAFIRISHAJI WA BIDHAA MUHIMU NA HUDUMA KATIKA NCHI ZA SADC KWA KIPINDI HIKI CHA JANGA LA VIRUSI VYA CORONA

Tarehe 6 Aprili, 2020 ulifanyika Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).  Mkutano huo ulijadili janga la mlipuko wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu (COVID-19) unaosababishwa na virusi vya Corona. Mkutano huo ulihusisha Mawaziri wenye dhamana ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Fedha,Viwanda,Biashara, Utalii, Mambo ya Ndani na Uchukuzi, kutoka nchi 16 wanachama wa SADC ambazo ni Angola, Botswana, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Jamhuri ya Visiwa vya Ushelisheli, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Zambia. Katika mkutano huo, Baraza la Mawaziri lilitoa mwongozo kuhusu Usafirishaji wa Bidhaa Muhimu na Huduma Katika Nchi za SADC katika kipindi hiki cha janga la Virusi vya Corona.  Mwongozo huu utatumika katika kipindi hiki unalenga kupunguza safari zisizo za lazima na usafirishaji wa bidhaa ambazo ni za muhimu tu na unazitaka Nchi Wanachama kuzingatia na kutekeleza sera na miongozo mbalimbali

Mambo muhimu ya kuzingatia unapohitaji kufanikiwa

Wengi wetu mara nyingi huwa tunafikiri kukosa mafanikio ni matokeo ya kukosa bahati katika maisha. Fikra hizo mara nyingi, huwazuia  wengi katika kufanikiwa na kujikuta wakiishia kuwa  watu wa kulaumu na kushindwa kila siku. Kimsingi  kitu kikubwa kinachochangia kuzuia mafanikio yetu ni baadhi ya tabia tulizo nazo. Si kweli kwamba watu wengi hushindwa kuendelea kutokana na kukosa mitaji bali ni kwa sababu ya tabia zao. Tabia ni kikwazo kikubwa cha maendeleo ya mtu binafsi kuliko unavyodhani. Zingatia haya yafuatayo ikiwa unahitaji kufanikiwa katika maisha yako:- Epuka kufikiria sana juu ya makosa uliyoyafanya. Kama kuna sehemu ulikosea katika siku za nyuma, hiyo imeshapita chukua hatu za kusonga mbele. Acha kutumia muda wako mwingi na kufikiri pale ulipokosea kwani hiyo haitakusaidia zaidi ya kukurudisha nyuma. Kumbuka kuwa kukosea ni sehemu ya maisha ya binadamu, kitu cha msingi jifunze kutokana na hayo makosa. Usiwe mtu wa kuongelea ndoto zako kila siku. Wengi