Skip to main content

Posts

Showing posts from March, 2020

Mchezaji wa Yanga aliesaini mkataba mpya wa miaka miwili

Mchezaji wa Yanga Bernald Morson Ameongeza Mkataba wa miaka miwili kuendelea kuwatumikia mabingwa wakihistoria kutoka Jangwani. Morson amesaini mkataba huo chini ya udhamini wa Kampuni ya GSM

Harmonize afunguka haya kuhusu H Baba kumkingia kifua na kujibizana na watu mitandaoni kisa yeye

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Harmonize ameweka wazi kuhusu kile anachokifanya msanii mwenzake wa Bongo Fleva ambaye pia yupo kwenye lebo ya Konde Gang H Baba kuonekana kumkingia kifua sana Harmonize na kufikia hatu hata kuwaongelea watu wengi na kuwakemea pale anapoona wanamuongelea au kumpiga vita Harmonize. Harmonize ameongea hayo akifanya mahojiano na kituo cha east Afrika Redio na majibu ya Harmonize yalikuwa hivi:”H Baba ni mmoja ya kaka zangu ambaye alinitangulia kwenye sanaa lakini suala na kupost na kufanya nini sijui huwezi kumpangia mtu maamuzi yake ile ni akaunti yake na anachokizungumza anazungumza kitu anachoona yeye kwake ni sahihi, Sasa ukitaka kumpangia mtu kwamba usipost hiki utakuwa kama unamuingilia maisha yake halafu ukiangalia mi mdogo tu nimeanza sanaa juzi tu, Itaonekana mdogo wangu we unanifundisha unajua mi nimepitia machungu mangapi?, Kwahiyo ni mtu ambaye namheshimu na nayaona anayepost kama unavyoona wewe”

Ujio mpya wa Chid Benz balaa, Akutana na Naibu Waziri wa Habari Shonza kuomba baraka na kuzungumza haya

Msanii wa bongofleva nchini Rashid Abdallah maarufu kama Chid Benz amemweleza Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza kuwa mapema wiki ijayo anatarajia kutoa video ya wimbo wake wa Beautiful na pia atatunga wimbo wa kuhusu Corona katika kikao kilichofanyika leo jijini Dodoma. Waziri Shonza amemhakikishia Chid Benz kuwa wizara ipo tayari kumpa ushirikiano wakati wowote na kikubwa ni msanii huyo kujituma na kuonyesha umma kwamba kweli ameachana na matumizi ya madawa ya kulevya.

Mwalimu chupuchupu kuuawa na wananchi, wenzake wamnusuru kwa kumfungia na kufuli ofisini

Mwalimu wa Shule ya Msingi Mitonji katika Kijiji cha Mitonji Kata ya Mbuyuni katika Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, John Mandanda amenusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kali, baada ya kuwacharaza viboko wanafunzi hadi mmoja kupoteza fahamu. Mwanafunzi huyo wa darasa la sita (jina linahifadhiwa) anadaiwa kupoteza fahamu kwa zaidi ya saa moja. Kutokana na tishio la kuchapwa na wananchi hao walimu walimwokoa mwenzao kwa kumfungia ndani ya ofisi, huku wananchi hao waliotaka kumpa kichapo wakiwa wamebeba marungu, mashoka na silaa zingine za jadi. Akizungumza na Nipashe jana kwa njia ya simu, Ofisa Elimu Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Elizabeth Mlaponi, alisema mwalimu huyo alifanya tukio hilo juzi majira ya saa 5:00 asubuhi wakati wanafunzi walipokuwa wakiingia darasani baada ya mapumziko mafupi. Alisema mwalimu huyo akiwa shuleni hapo siku ya tukio, alitoa adhabu kwa baadhi ya wanafunzi ambao inaelezwa kuwa wanafunzi hao walikuwa wamechelewa kuingia darasani

Lukaku aeleza alivyokataa ombi la Solskjaer la kubaki Man United

Mshambuliaji wa zamani wa Man United anayeichezea club ya  Inter Milan ya Italia Romelu Lukaku ameweka wazi kuwa kocha wa Man United Ole Gunnar Solskjaer alimtaka asiondoke katika club hiyo ili aendelee kuitumikia Man United. “Ilikuwa ni hali ngumu kwangu na nilitakiwa nifanye maamuzi ya kwenda sehemu ambayo naweza kujifunza vitu vingine kuhusiana na uchezaji wangu na kufanya kazi na mtu ambaye ananihitaji, Ole alinitaka nibaki lakini nilimwambia kuwa nimemaliza”>>> Lukaku Lukaku aliondoka  Man United 2019 baada ya kukaa katika club hiyo kwa miaka miwili lakini hakuwa na wakati mzuri sana kama ilivyokuwa kwa Inter Milan, Lukaku aliishawishi Man United imsajili 2017 kufuatia kiwango chake cha kucheka na nyavu alichokionesha Everton lakini ikawa tofauti akiwa Man United.