Skip to main content

Posts

Showing posts from April, 2020

HIZI HAPA FAIDA ZA KULA TANGO

Matango yanashika nafasi ya nne kwa kulimwa katika aina ya mbogamboga zinazolimwa duniani kote na tunda hili linafahamika kuwa miongoni mwa vyakula bora kwa afya yako maranyingi yanaitwa superfood. JINSI YA KUCHAGUA TANGO BORA KWA AFYA YAKO 1.Angalia tango lenye rangi ya kijani mkozo(dark green) 2.Angalia tango ambalo bado ni ligumu vizuri halijalegea(firm). Baada ya kuchagua tango osha vizuri kwa maii safi sasa unaweza kulitumia kwenye kachumbari,au kwa kulikata na kula hivyovyo,pia kutengenezea juisi FAIDA ZA KUTUMIA MATANGO 1.Kuupatia mwili maji ya kutosha Kwa wale ambao ni wavivu au wako busy sana hata kupata muda wa kunywa maji ya kutosha inakuwa ngumu,Tafuta matango ya baridi ambayo asilimia tisini ni maji,Yatasaidia kurudisha maji yaliyopotea mwilini 2.Husaidia kupambana na joto kali ndani na nje ya mwili Kula tango husaidia kupunguza joto kali ndani ya mwili(heartburn) na pia kupaka kwenye ngozi kutakusaidia kpunguza kuungua na jua 3.Huondoa sumu mwilini(toxins

MWONGOZO WA USAFIRISHAJI WA BIDHAA MUHIMU NA HUDUMA KATIKA NCHI ZA SADC KWA KIPINDI HIKI CHA JANGA LA VIRUSI VYA CORONA

Tarehe 6 Aprili, 2020 ulifanyika Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).  Mkutano huo ulijadili janga la mlipuko wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu (COVID-19) unaosababishwa na virusi vya Corona. Mkutano huo ulihusisha Mawaziri wenye dhamana ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Fedha,Viwanda,Biashara, Utalii, Mambo ya Ndani na Uchukuzi, kutoka nchi 16 wanachama wa SADC ambazo ni Angola, Botswana, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Jamhuri ya Visiwa vya Ushelisheli, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Zambia. Katika mkutano huo, Baraza la Mawaziri lilitoa mwongozo kuhusu Usafirishaji wa Bidhaa Muhimu na Huduma Katika Nchi za SADC katika kipindi hiki cha janga la Virusi vya Corona.  Mwongozo huu utatumika katika kipindi hiki unalenga kupunguza safari zisizo za lazima na usafirishaji wa bidhaa ambazo ni za muhimu tu na unazitaka Nchi Wanachama kuzingatia na kutekeleza sera na miongozo mbalimbali

Mambo muhimu ya kuzingatia unapohitaji kufanikiwa

Wengi wetu mara nyingi huwa tunafikiri kukosa mafanikio ni matokeo ya kukosa bahati katika maisha. Fikra hizo mara nyingi, huwazuia  wengi katika kufanikiwa na kujikuta wakiishia kuwa  watu wa kulaumu na kushindwa kila siku. Kimsingi  kitu kikubwa kinachochangia kuzuia mafanikio yetu ni baadhi ya tabia tulizo nazo. Si kweli kwamba watu wengi hushindwa kuendelea kutokana na kukosa mitaji bali ni kwa sababu ya tabia zao. Tabia ni kikwazo kikubwa cha maendeleo ya mtu binafsi kuliko unavyodhani. Zingatia haya yafuatayo ikiwa unahitaji kufanikiwa katika maisha yako:- Epuka kufikiria sana juu ya makosa uliyoyafanya. Kama kuna sehemu ulikosea katika siku za nyuma, hiyo imeshapita chukua hatu za kusonga mbele. Acha kutumia muda wako mwingi na kufikiri pale ulipokosea kwani hiyo haitakusaidia zaidi ya kukurudisha nyuma. Kumbuka kuwa kukosea ni sehemu ya maisha ya binadamu, kitu cha msingi jifunze kutokana na hayo makosa. Usiwe mtu wa kuongelea ndoto zako kila siku. Wengi